Bodi ya Bima ya Amana, ijulikanayo kama Deposit Insurance Board (DIB) ni taasisi yenye jukumu la kukinga amana katika benki na taasisi za fedha hapa Tanzania. DIB: “Tunakinga Amana yako”
Ulipaji wa Fidia kwa wenye Amana
Jukumu la Bodi ya Bima ya Amana ni kuwalinda wenye amana dhidi ya athari ya kupoteza amana zao pale benki au taasisi ya fedha inapowekwa katika ufilisi
Usimamizi wa Mfuko wa Bima ya Amana
Bodi ya Bima ya Amana inakusanya michango ya kila mwaka kutoka benki na taasisi za fedha
Kutoa elimu kwa Umma
Bodi ya Bima ya Amana inatoa elimu kwa umma katika jitihada za kukuza uelewa wa majukumu ya Bodi yetu. Elimu kwa umma ni moja ya nguzo muhimu za IADI ambayo inasema ni muhimu kwa umma kuelezwa mara kwa mara kuhusu faida za mfumo wa bima ya amana pamoja na ukomo wake.
Dhima
Dhima ya Bodi ya Bima ya Amana (DIB) ni kuchangia katika kuujengea uimara, uadilifu na imani kwa jamii, mfumo wa fedha nchini kwa kutoa kinga (bima) kwa amana stahili
Dira
Kuwa taasisi inayoaminika katika kukuza uthabiti na kujenga imani kwa umma katika mfumo wa fedha.
Tunu
- Uadilifu: Tunazingatia viwango vya juu vya uadilifu katika kutekeleza majukumu yetu tukiongozwa na dhima yetu.
- Uwajibikaji: Tunatekeleza majukumu yetu kwa uwazi na kuwajibika kwa wadau wetu.
- Mawasiliano: Tunawasiliana na kushirikiana na wadau wetu kikamilifu.
- Utendaji wa pamoja: Tunazingatia utendaji kazi wa pamoja katika nyanja mbalimbali
- Ubora: Tunatimiza majukumu yetu kwa weledi na kuzingatia ubunifu katika kuboresha utendaji kazi.
News and Updates
TAARIFA KWA UMMA 02-17-2023
BODI YA BIMA YA AMANA TAARIFA KWA WADAI - INARUDIWA KATIKA SHAURI LA UFILISI WA BENKI ZA GREENLAND BANK (T)