Kuhusu DIB

Bodi ya Bima ya Amana – DIB

Bodi ya Bima ya Amana (DIB) ni taasisi iliyoanzishwa kwa mujibu wa kifungu Na. 37 (1) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya 2006. Bodi ina wajibu wa kutunga sera, kusimamia na kudhibiti Mfuko wa Bima ya Amana.

  • Malengo ya Bodi ni pamoja na;

    • Kutoa kinga dhidi ya upotevu wa sehemu au amana zote za wenye amana katika benki
      na taasisi za fedha.
    • Kuchangia katika kuleta utulivu katika mfumo wa fedha nchini Tanzania.
  • Kuanzishwa kwa DIB

    Bodi ya Bima ya Amana (DIB) ni taasisi iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha Na. 5 ya mwaka 2006 sehemu ya VII kifungu cha 36 hadi 42.

  • Historia ya Bima ya Amana

    Kwa mara ya kwanza Bima ya Amana ilianzishwa nchini Marekani mwaka 1933 kufuatia Mdororo Mkubwa wa Kiuchumi. Kuanzia wakati huo Bima ya Amana imenzishwa katika nchi zaidi ya 100, ikiwa ni pamoja na Nigeria, Kenya, Zimbabwe, Uganda, Rwanda, Uingereza, Kanada, Ufaransa, Japani, Ufilipino, Korea Kusini na Taiwani.