Bodi ya Wakurugenzi

Bodi inawajibika kwa kutengeneza sera zinazolenga kuhakikisha usimamizi na udhibiti wa DIF unafanyika kwa ukamilifu na ufanisi. Kwa mujibu wa sheria, Bodi ya DIB inajumuisha wajumbe wafuatao: Gavana wa BOT – Mwenyekiti; mwakilishi mmoja kutoka Wizara ya Fedha na Mipango (MoFP); Katibu Mkuu, Hazina Ofisi ya Rais ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar; na wajumbe wengine watatu walioteuliwa na Waziri wa Fedha.