Close

TAARIFA KWA UMMA 02-17-2023

BODI YA BIMA YA AMANA

TAARIFA KWA WADAI – INARUDIWA

KATIKA SHAURI LA UFILISI WA BENKI ZA GREENLAND BANK (T) LIMITED NA DELPHIS BANK (T) LIMITED ZILIZO CHINI YA UFILISI WA BODI YA BIMA YA AMANA

Kwa muda mrefu Bodi ya Bima ya Amana imekuwa ikiendelea na ufilisi wa  Greenland Bank (T) Limited na Delphis Bank (T) Limited zilizofungwa mnamo mwaka 2000 na 2003 kwa kukusanya mali ikiwemo mikopo kutoka kwa wadaiwa, ulipaji wa fidia ya bima ya amana,ulipaji wa fidia ya ufilisi pamoja na kuhudhuria kesi mbalimbali za benki husika kwa mujibu wa sheria ya Benkienki na Taasisi za Fedha ya Mwaka 2006.

Hivyo basi kutokana na sababu mbalimbali zinazosababisha kukosekana kwa makusanyo kutoka kwa wadaiwa wa benki husika, notisi inatolewa kwa wadau wa benki hizo kuhudhuria vikao mnamo tarehe 24 Machi 2023, kuanzia saa 04:00 asubuhi kwa benki ya Greenland (T) Limited na tarehe 24 Februari 2023 kuanzia saa 08:00 mchana kwa benki ya Delphis (T) Limited vitakavyofanyika katika Jengo la ofisi za  Benki Kuu ya Tanzania, Ofisi ndogo ya Makao Makuu Dar es Salaam, ili kujadili ajenda zifuatazo:

  • Kujadili na kukubaliana kuhusu ripoti za mwisho za ufilisi .
  • Kuunda Kamati za Wadai (Creditors Inspection Committees) na kupata idhini zao kuhusu ugawaji wa fidia ya ufilisi kwa kiasi kilichopo kwa wadai wa Greenland Bank (T) Limited na Delphis Bank (T) Limited kwa mujibu wa Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya Mwaka 2006 .

 

Mkurugenzi

Imetolewa tarahe 08 Machi 2023

GREENLAND ADVERT ZANZIBAR LEO 02-17-2023

Related Posts