Close

TAARIFA KWA WADAI 29-Dec-2023

KATIKA SHAURI LA FBME BANK LIMITED (ILIYO CHINI YA UFILISI)

 TAARIFA KWA WADAI

 BODI YA BIMA YA AMANA (Deposit Insurance Board-DIB) ambayo ni Mfilisi wa Benki ya FBME imited inatoa taarifa kwa umma na kwa wadai wote wa benki hiyo kuwa muda wa kuwasilisha madai umeongezwa kwa muda wa miezi miwili kuanzia tarehe 1 Januari hadi 29 Februari 2024 na kuwa:

  • Wadai wa Tanzania wenye amana (local depositors) zaidi ya shilingi milioni moja na laki tano (1,500,000/=) dhidi ya FBME Bank Limited (ambayo iko chini ya ufilisi) kuwasilisha madai kwa Mfilisi (DIB) katika ofisi za benki hiyo tawi la Samora, Dar es Salaam (jengo la TSN) au ofisi za Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Zanzibar, Arusha au Mwanza, yakiwa na uthibitisho kamili kwa kutumia fomu maalumu ya madai iliyojazwa kikamilifu ikiambatishwa na nakala ya kitambulisho kinachotambulika kitaifa.
  • Vile vile, wadai wengine ambao sio wenye amana (other creditors) wanataarifiwa kuleta madai yao yakiwa na uthibitisho kamili kwa kutumia fomu ya madai ikiambatishwa na nakala ya kitambulisho kinachotambulika kitaifa.
  • Fomu ya madai inapatikana katika ofisi za FBME Bank Limited mtaa wa Samora, Dar es Salaam, Ofisi za DIB zilizoko ghorofa ya 11 Mnara wa Kaskazini, BOT Dar es Salaam, matawi yote ya BOT na kwenye tovuti ya DIB: dib.go.tz.
  • Wateja wa kimataifa (TIB depositors) wawasilishe madai yao kwa PETROS IOANNIDES, ambaye ni Mfilisi wa tawi la FBME Bank Limited, Cyprus na wakala wa DIB nchini Cyprus. Maelekezo ya Bw. Petros kuhusu uwasilishaji wa madai ya wateja hao yanapatikana kwenye tovuti ya benki ya FBME (fbmeliquidation.com ) au kwa kuwasiliana naye kwa barua pepe kupitia: customer.service@fbme.com or kupitia barua kwenye anwani 3 Agiou Prokopiou street, 2406 Engomi, Nicosia, Cyprus au P O Box 25566, 1391 Nicosia, Cyprus.

 Imetolewa tarehe 29 Desemba 2023.

TAARIFA KWA WADAI WA FBME BANK DIB

Related Posts