SHAURI LA FBME BANK LTD
KATIKA SHAURI LA FBME BANK LTD (ILIYO CHINI YA UFILISI)TAARIFA KWA WADAI
BODI YA BIMA YA AMANA (Deposit Insurance Board-DIB) ambayo ni Mfilisi wa Benki ya FBME Ltd inatoa taarifa kwa umma na kwa wadai wote wa benki hiyo kama ifuatavyo:
(a) Wadai wa Tanzania wenye amana (local depositors) zaidi ya shilingi milioni moja na laki tano (1,500,000/=) dhidi ya FBME Bank Ltd (ambayo iko chini ya ufilisi) kuwasilisha madai kwa Mfilisi (DIB) katika ofisi za benki hiyo tawi la Samora, Dar es Salaam (jengo la TSN) au ofisi za Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Zanzibar, Arusha au Mwanza, yakiwa na uthibitisho kamili kabla ama kufikia tarehe 29 Disemba 2023 kwa kutumia fomu maalumu ya madai iliyojazwa kikamilifu.
(b) Vile vile, wadai wengine ambao sio wenye amana (other creditors) wanataarifiwa kuleta madai yao yakiwa na uthibitisho kamili kwa kutumia fomu ya madai.
(c) Fomu ya madai inapatikana katika ofisi za FBME Bank Ltd mtaa wa Samora, Dar es Salaam, Ofisi za DIB zilizoko ghorofa ya 11 Mnara wa Kaskazini, BOT Dar es Salaam, matawi yote ya BOT na kwenye tovuti ya DIB: www.dib.go.tz
(a) Wateja wa kimataifa (TIB depositors) wawasilishe madai yao kwa Bw. PETROS IOANNIDES, ambaye ni Mfilisi wa tawi la FBME Cyprus na wakala wa DIB nchini Cyprus. Maelekezo ya Bw. Petros kuhusu uwasilishaji wa madai ya wateja hao yanapatikana kwenye tovuti ya benki ya FBME (fbmeliquidation.com ) au kwa kuwasiliana naye kwa barua pepe kupitia: customer.service@fbme.com
Imetolewa tarehe 21 Novemba 2023:
Mkurugenzi,
Bodi ya Bima ya Amana,
Jengo la Benki Kuu ya Tanzania, Ghorofa 11,
2 Mtaa wa Mirambo 11884, Box 2939 Dar es Salaam
Email: DIB – INFO@bot.go.tz
Tel: +255 22 223 5390